NYOTA YA SIMBA ( LEO)

Hii ni nyota ya Tano katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 Julai hadi 22 Agosti au wenye majina yanayo anza na herufi E au Q au S au T.
Usawa wake ni Dume.
Asili yake ni Moto.
tabia yake ni thabiti
Sayari yake ni Jua(Sun).
Siku yake nzuri ya bahati ni siku ya Jumapili,
Namba ya bahati ni 1,3,10,19 na 4 .
Malaika wake anaitwa Michael au Raukayaeel
Jini anayetawala Jumapili anaitwa Abdulahi Saeed al Madhhab au Och.
Rangi zao ni rangi ya Dhahabu (Gold), Nyekundu (Red) na rangi ya Machungwa (Orange)
NGUVU YA NYOTA HII
Wenye nyota hii huwa na nguvu ya Ubunifu, shauku, ukarimu, moyo safi, furaha, wenye kupendelea kucheka,
UDHAIFU WA NYOTA HII
kiburi, ukaidi,kujitegemea,uvivu, asiye na akili.
WANACHOPENDA
wenye nyota hii hupenda sana maeneo yenye kujichanganya kwa watu kujionyesha,kuchukua likizo,kupenda mambo makubwa ya gharama,rangi zenye kuwaka,na kujifurahisha na marafiki.
WASICHOPENDA
Kupuuzwa,kukubaliana na hali,kutokutukuzwa kama mfalme au malkia.
MAMBO MENGINE KUHUSU WAO
Wenye nyota hii ni watu wenye bahati sana hasa kulingana na nyota yao, katika maswala ya kiuchumi, japo kuwa ni nyota ya watu wenye kutumia sana pesa hovyo na inayeyuka kama vile moto.
mara nyingi huwa na marafiki wengi kutokana na kuwa na ukarimu na uaminifu, hii ni kama vile jua linavyounganisha sayari nyingi na kuwa source ya nishati, na hisia zao za ucheshi ndio huwafanya kuwa karibu zaidi na watu wengi sana.
Watu wote wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake nyumba zao au magari yao rangi zilizochangamka na zenye kuonyesha utajiri kama Dhahabu na Njano nzito au iliyoiva.
Rangi zinazowapa uwezo wa Mapenzi, Mahaba na Furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Nyeusi,
ambayo hiyo mara nyingi hufaa zaidi siku ya jumamosi
ambazo pia hufaa zaidi siku ya Alhamisi.
Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni, Njano (Yellow) na Njano-Machungwa.
ambayo inamfaa zaidi akivaa siku yake ya bahati.
Kito (Jiwe) ni Amber,Ruby,Chrysolite, Yellow Diamond, Petrified Wood Garnet, Diamond, Jasper, Quartz na Onyx.
kila kito kina kazi maalum kwake. lakini kito kikuu kwake ni Ruby.
Madini yao ni Gold (Dhahabu). Manukato yao ni Miski (Musk) na Uvumba.
MAMBO MUHIMU:-
Sifa ya Nyota hii ni Uimara na Kutokubadilika.
Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni Unyenyekevu.
Maadili yao ni Uwezo wa Uongozi, Kujiamini, Ukarimu, Ubunifu na Kupenda raha.
Matakwa yao ni Starehe, Haja ya Kung’ara mbele za watu na Kujikweza.
Tabia za kujiepusha nazo ni Kujisifu, Kiburi na Kuamrisha.
USHIRIKIANE NA NANI?
Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Punda na Mshale.
Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Ng’ombe, Nge na Ndoo.
Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Ng’ombe.
Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Nge.
Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mashuke.
Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Mshale.
Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Ndoo.
Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Mshale.
Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Punda na Kaa.
KIPAJI CHA SIMBA
Simba wana kipaji cha ufunuo wa kiungu , wana uwezo wa kuvumbua mambo ambayo yanaweza kuwaletea fedha pamoja na kwamba hazikai.Wanauwezo vilevile wa kuponya kwa kutumia mikono yao kuponya watu na wanakipaji cha asili cha uongozi. (inspired):TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI
Simba ni watu wanaopenda ufahari mkubwa na kutukuzwa. Wanapenda kutumia na wanataka waonekane kwamba wana hali nzuri, wanapenda sana kuheshimiwa.watu hawa huwa ni wakali sana katika mapenzi na mara nyingi huwa hawadumu kwenye mapenzi kutokana na ukali wao na huwa ni watu wenye ghadhabu za mara kwa mara hasa akikosewa au akipingwa kidogo tu, kimapenzi.
Ni watu wakarimu lakini wajeuri na wanapenda sana kuonea watu. Wana hisia kali, ni wakali na wanakiburi.Tabia yao ni kujitanua, Ukarimu na ulezi ikichanganyika na ujeuri na kujionyesha, huwaharibu wale wanaowapenda.
Furaha haina mpaka katika mapenzi ya Simba, mioyo yao mikubwa na hisia zao nzito hutokeza dhahiri wanapompenda mtu. Baada ya hapo ndipo sura kamili ya Simba hujitokeza.
Wao wanathamini sana mapenzi na juu ya jambo lolote, na wanaweza kuwa waaminifu sana na wakati mwingine huwaabudu wapenzi wao.Wanapenda kujishughulisha sana na mambao ya mapenzi lakini mambo yakiharibika inakua vigumu sana kuyatengeneza.
Tatizo lao kubwa ni kujisahau Kwa nje wanaonekana ni wenye kujiamini katika mapenzi lakini kwa ndani wanaweza kuwa wanaumia lakini hawawezi kukubali. Hata hivyo mara nyingi hutegemea kupata hisia kama walizonazo wao kutoka kwa wapenzi wao.
KAZI NA BIASHARA ZA SIMBA
Wenye nyota hii wanatakiwa wafanye kazi zifuatazo; kazi za usimamizi, kama katika kampuni yake binafsi au katika mashirika au biashara, kazi za michezo au uongozi wa michezo.MAVAZI NA MITINDO
Simba mitindo yao iwe ya kifalme, Kitajiri na inayoashiria nguvu na mamlaka, Kitambaa kiwe cha hariri inayongaa au velvet au kilicho tariziwa, Rangi iwe ya Dhahabu.MAGONJWA YA SIMBA
Nyota hii inatawala moyo, sehemu ya juu ya mgongo na bandama.Vilevile inatawala uti wa mgongo na mshipa mkubwa wa damu.VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA SIMBA
Wenye nyota hii wanatakiwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao, machungwa, maboga, vitu vichachu kama ndimu au malimao na wapende sana kula nyama za ng'ombe, mbuzi na kondoo.MADINI, VITO NA MAFUSHO
Madini ya Simba ni Dhahabu. Vito vyao vya kuvaa katika pete ni Peridot au RubyMafusho ya Simba ni Sandarusi unachoma siku ya Jumapili kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.
FUNGUO
Funguo ya simba ni "nita" anaposema atapata au atafanya basi kitu hicho hukipata,
Wasiliana nasi
Ikiwa ni mwenye kupendezewa na makala hizi, basi jihisi huru kuendelea kutufuatilia kupitia email lakini pia kama unahitaji mawasiliano yetu, tunapatikana kwa ajili ya misaada ya mfano wa makala hizi.
Unaweza kutupata kwa kupitia Email, vile vile kwa namba za simu, kupitia fomu ya mawasiliano katika tovuti yetu. Msaada wa kirafiki zaidi unatolewa na team yetu ya huduma kwa wateja na kujibu maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo,
Ikiwa una maswali kuhusu makala zetu pia unaweza kuacha kwenye comment katika makala husika na kama ni huduma ya msaada wa tiba za kiroho au ushauri ama unahitaji kuagiza ama una suala lolote lingine basi tupo kwa ajili ya kutoa msaada pia.
Usisite kuwasiliana nasi kwa hekima za mawasiliano nifuraha yetu kusikia mahitaji ya wateja ama rafiki wa tovuti zetu za unajimu na RakimsSpiritual na tunatoa huduma nzuri za kumridhisha mwenye shida ikiwa tu atakidhi vigezo vya kuwa mteja ama rafiki wa tovuti hizi asante.
Na kwa maswali ya dharula kuhusiana na makala zetu kwa Members pekee;
Jihisi huru kututafuta masaa 24 ya week kupitia:-
Rakimsspiritual@gmail.com au mnajimu@unajimu.com
WhatsApp number
Rakims
Unaweza kutupata kwa kupitia Email, vile vile kwa namba za simu, kupitia fomu ya mawasiliano katika tovuti yetu. Msaada wa kirafiki zaidi unatolewa na team yetu ya huduma kwa wateja na kujibu maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo,
Ikiwa una maswali kuhusu makala zetu pia unaweza kuacha kwenye comment katika makala husika na kama ni huduma ya msaada wa tiba za kiroho au ushauri ama unahitaji kuagiza ama una suala lolote lingine basi tupo kwa ajili ya kutoa msaada pia.
Usisite kuwasiliana nasi kwa hekima za mawasiliano nifuraha yetu kusikia mahitaji ya wateja ama rafiki wa tovuti zetu za unajimu na RakimsSpiritual na tunatoa huduma nzuri za kumridhisha mwenye shida ikiwa tu atakidhi vigezo vya kuwa mteja ama rafiki wa tovuti hizi asante.
Na kwa maswali ya dharula kuhusiana na makala zetu kwa Members pekee;
Jihisi huru kututafuta masaa 24 ya week kupitia:-
Rakimsspiritual@gmail.com au mnajimu@unajimu.com