Mahusiano kinyota ya Punda na Punda (Aries and Aries Compatibility) 1

Rakims

Mahusiano kinyota ya Punda na Punda 

(Aries and Aries Compatibility)

 Kama katika usemi wa Mshahiri mahiri  William Schwenck Gilbert alivyosema mapenzi yanazungusha Dunia. 

Mahusiano kinyota ya Punda na Punda
Mahusiano kinyota Punda na Punda/Aries & Aries

Basi katika playlist hii tutaangalia mahusiano kinyota baada ya kuwa tumeangalia sifa za kila nyota katika playlist iliyopita.

Basi hapa utatambua na kuelewa zaidi kuhusu mahusiano ya kila nyota na nyota nyingine na hata hivyo bila kusahau kila jinsia moja na nyingine katika nyota basi huwa na mtizamo tofauti katika mapenzi au namna ya kuyaendea mapenzi hata katika ladha ya kufanya tendo.

Basi kwa hapa bila kupoteza muda na bila kuchelewa basi tutaanza na nyota mbili ambazo ni Punda/Kondoo yaani Aries pamoja na Aries.

Yes yani tunazungumzia mahusiano kinyota kati ya Punda na Punda maelezo zaidi unaweza kuendelea kwenye video hii chini 👇


Fahamu ya kuwa ikiwa wewe una nyota ya Punda na mwenza wako ananyota ya Punda basi Jua wawili nyinyi ni fahari wawili wenye asili sare ndio maana hata mkiomkionana utakuta ni wale wanaitwa love at first sight kwamba wenye kupendana wakionana tu mara ya kwanza, 

kwa maana wewe ni moto wa mlipuko na yeye pia hivyo hivyo katika mtizamo tunasema;

Mapenzi yenu ni makali na moto mkali ambao unaweza kuunguza chochote lakini ukikosa cha kuunguza mnaunguzana wenyewe. 
Nikiwa na maana kati yenu mapenzi yenu ni sawa na mbio za riadha au vita kila mtu anataka ushindi, challenges na utawala nani awe juu ya mwenzie ni jambo litakalo kuwa katika roho ya kila mtu japo mnaweza kufichana katika nyama.

Kuna vitu mwenza wako atakuwa anafanya unaona kabisa huyu anafanyia ushindani, Hivyo nyie ni pacha kweli wa kinyota lakini ni kama time bomb any second! utaskia kabooom!!!

Vyote mnakuwa mnaendana kasoro kwenye issue ya uaminifu na sex hapo tu ndio kuna vita pia migogoro yenu itapungua kama kila mtu nguvu zake atawekeza nje na hasira. 

Vile vile ni watu mkikutana basi pesa na bahati hufunguka baada ya kufanya tendo hata hivyo ni watu mnaweza kutumia pesa inayayuka kama moto na pesa ikiisha ndio roho zinatulia.

Mnaendana vizuri ila mtakamilika kama yeye au wewe mmoja wenu akijishusha nje ya hapo nyie vita yenu hamna wa kuizima. 

Hizi ndoa mara nyingi wahusika sauti zao huwa kama zimeharibikia kwenye max volume yaani mtu aliongeza sauti kisha switch ya sauti ikaharibikia huko any second ni moto tu.
Mkianza kuongea ni sawa na wayahudi wanataka kuua mtu.

NOTE:
Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:


Gharama sh elfu 10,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: 
+255 783 930 601

Rakims Spiritual

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !