Ambayo historia hiyo huenda ndio ikawa historia iliyofanya nyota hiyo kupewa jina husika.
Katika makala hii tutaangalia historia ya nyota ya samaki kwa ufupi sana;
Nyota ya Samaki maarufu kama Pisces ni nyota ya 12 katika mlolongo wa nyota 12 za unajimu.
Nyota hii kimtizamo ni kwa watu waliozaliwa katika ya tarehe 19 Februari na Machi 20
unaweza kuisoma zaidi kwenye makala hii
https://rakimsspiritual.com/2021/03/nyota-ya-samaki-pisces/
Hawa ni samaki wanaoogelea pamoja inaaminika kwamba historia yao walikuwa wamefungwa mikia na wanaogelea sehemu mbili tofauti;
Maarufu katika lugha ya kichina kama Yin na Yang

Yin yang ni mfano wa vitu viwili tofauti vyenye kwenda sawa kwa kutegemeana mfano;
- hasi na chanya
- usiku na mchana
- jua na mwezi
- moto na upepo
- maji na udongo
Na hili suala lilikuwa likichukuliwa hivyo zamani sana kama miaka 2000 kabla ya kuzaliwa Christ watu wa Babilon pia waliona kitendo hicho na baadae wakaanza kutangaza kuwa ikiashiria hivyo basi ni vita za ndani na watoto watakaozaliwa chini ya tukio hilo basi watakuwa wamezaliwa chini ya maarifa hayo na watakuwa ni watu wasiri na wenye vita za ndani,
lakini baadae ilikuja kufahamika kuwa hili tukio likitokea samaki hao kufanya hivyo basi sababu yake huwa ni nyota 12 angani zikikaa katika mfumo huo,
hapo ni baada ya wapima magimba kuanza ugunduzi lakini historia nyingine huwa inasema kuwa Wagiriki walikuwa wakiita kitendo hicho kuwa ni kitendo cha miujiza kinachohusishwa na Zahara/Zuhura na Cupid(mungu wa kigiriki wa mapenzi) ya kwamba
Kulikuwa na mnyama aina ya Dragon aliyeitwa Typhon mwenye vichwa 100 na macho yanayowaka moto,akiwa na sauti ya nyoka, chini kidogo akiwa na umbo la ng'ombe na sauti ya ngurumo kama simba,
siku moja Zuhura na mwanawe Cupid walikuwa wakitembea jirani na mto mwembamba wa Euphrates pichani

akatokea huyo Typhon na kuwaachamia ulimi wake mweusi wenye kuwaka moto basi Zuhura alivyoona hana nguvu tena kwa woga akamuita baba yake Mushtar ambayo sasa hivi ni jina la sayari na baba yake huyo kwa haraka sana akawageuza na kuwa samaki wakaingia kwenye maji na kuogelea na kukimbia
Lakini hadithi nyingine inasema kuwa pale walitokea samaki wawili ambao ndio hao waliokuwa wakiogelea wawili kuonyesha vita za ndani na usiri wakawakomboa na kukimbia kwenye maji.
akatokea huyo Typhon na kuwaachamia ulimi wake mweusi wenye kuwaka moto basi Zuhura alivyoona hana nguvu tena kwa woga akamuita baba yake Mushtar ambayo sasa hivi ni jina la sayari na baba yake huyo kwa haraka sana akawageuza na kuwa samaki wakaingia kwenye maji na kuogelea na kukimbia
Lakini hadithi nyingine inasema kuwa pale walitokea samaki wawili ambao ndio hao waliokuwa wakiogelea wawili kuonyesha vita za ndani na usiri wakawakomboa na kukimbia kwenye maji.
Sasa kama zawadi hao samaki ndio wakarushwa juu ya anga na kujipanga pamoja na hizo nyota 12 na kuanzia hapo ndio wakawa hawaonekani na zinaonekana nyota peke yake.kila ikifikia kipindi hicho.
ndio maana kwa utafiti wakaja kugundua kuwa kila anaezaliwa chini ya nyota hizo huwa na mambo hayo ya sifa za hiyo nyota.
Nakwambia hii story sio nakuaminisha haya hapana nakwambia ili ujue sababu ya hizo nyota kuitwa majina hayo tofauti na Nguruwe na fisi ni kuwa wana historia ya kuitwa hivyo lakini ukitaka unaweza kugeuza jina la nyota yako ikawa chambo ila maelezo uyajue kuwa yanabase na nini ndio maana wachina kujionyesha kuwa wanajua sana story hii wakawaita miungu wao wawili Yin & Yang
wakiashiria samaki wawili walipoanza kuwaabudu ikabidi wageuze jina la nyota ya samaki kuwa nguruwe
Hii historia ipo katika uandishi zaidi bado hivyo kama utahitaji kuisoma baadae usisite kusubscribe kupitia email na itakapo kuwa teyari utaipata kwa ukamilifu.
Rakims